Wachezaji hao ambao mpaka sasa hawajatajwa na kocha mkuu Antonio Conte, watafanyiwa vipimo vya PCR kuona kwamba kama kutakuwa na wagonjwa zaidi na kuthibithisa ripoti za madaktari ilikuweza kuwakinga wengine ambao watakosa mchezo wa kwanza na wapili katika nusu fainali.
Kwa mara ya kwanza Conte atarudi Stamford Bridge siku ya Jumatano Januari 5, baada ya kuondoka Chelsea mwaka 2018, kutokana na kushindwa kumaliza nafasi nne za juu licha ya kushinda Kombe la FA msimu huo wa 2017/ 2018 ikiwa ni msimu mmoja baada ya kushinda taji la Ligi kuu msimu wa 2016/2017.
Muitaliano huyo anatazamia kuipa Tottenham taji la kwanza tangu mwaka 2008 waliposhinda kombe la ligi kwenye fainali dhidi ya Chelsea.


