
Mserbia huyo ambae ameshinda mataji 5 ya ligi kuu ya uingereza pamoja na lile la klabu bingwa ulaya katika miaka yake 8 aliyokipiga Old Trafford,amesema kuwa majeraha yamemfanya atundike daluga.
Vidic mwenye umri wa miaka 34 alilazimika kuachana na Inter Milan mwezi huu baada ya kushindwa kucheza mchezo wowote kwenye seria A msimu huu.
Vidic alijiunga na United akitokea Spartak Moscow mwezi January 2006, ambapo alifanya vizuri kwenye safu ya ulinzi akishirikiana na Rio Ferdinand jambo ambalo lilianza kumpa mataji mfululizo kocha wa wakati huo Sir Alex Ferguson aliyenyakua mataji matatu mfululizo kati ya mwaka 2007 na 2009 ambapo pia ndani ya mwaka 2008 alinyakua taji la mabingwa wa ulaya.