Wasanii wa kiume hawajui kuvaa bongo

Alhamisi , 4th Jul , 2019

Mbunifu wa mavazi hapa nchini Tanzania Martin Kadinda, amewachana wasanii wa kiume na mastaa wa bongo kuwa hawajui kuvaa.

Martin Kadinda

Martin Kadinda amesema hayo kupitia EATV&EA Radio na Digital, wakati alipokuja kuchangia harambee ya Namthamini kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa pedi kwa watoto wa kike waliopo shuleni.

"Wapo wengi na wana majina makubwa, wenyewe wanajiamini wanaweza acha wabaki hivyo hivyo, na wakiume ndio wanaharibu kabisa bora hata wa kike. Wasanii wa kike wanajitahidi kuvaa kuliko wakiume."

Aidha Mbunifu huyo wa mitindo amesema anavutiwa na mavazi ya Vanessa Mdee kwa upande wa kike, na Gnako Warawara kwa upande wa kiume.

Pia ametoa ushauri juu ya mavazi ya kuvaa katika kipindi hiki kuwa ni yale yenye aina ya pamba, na tuachane na mavazi ya ngozi.