
Stephen Curry amefunga alama 32, ametoa Assist 8 na Rebound 5.
Ushindi huu unaifanya Golden State kuongoza kwa ushindi wa michezo 3-1 kwenye michezo 4 ya nusu fainali waliocheza. Katika mchezo huu Stephen Curry amefunga alama 32, ametoa pasi za kufunga (Assist) 8 na Rebound 5.
Mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa leo Alfajiri ukanda wa Mashariki Boston Celtics wameinyuka Milwaukee Bucks kwa ushindi wa alama 116 kwa 108. Na kufanya timu hizi zote kuwa zimeshinda michezo 2 kila timu katika michezo 4 waliocheza.
Kwenye mchezo huu mchezaji nyota wa Celtics Al Horford amefunga alama 30 (Assists) 3 na rebound 8. Jayson Tatum amefunga alama 30, pasi za kufunga (Assists) 5 na rebound 13. Na mchezaji nyota wa Bucks Giannis Antetokounmpo amefunga alama 34 ametoa pasi za kufunga (Assists) 5 na Rebound 18.