Jumapili , 13th Jan , 2019

Uongozi wa klabu ya Yanga umeutolea ufafanuzi ujumbe wa kiungo wake Mzimbambwe, Thabani Kamusoko baada ya kuleta sintofahamu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Thabani Kamusoko.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari, Dismas Ten, ametoa ufafanuzi kuwa Kamusoko aliandika na hakuwa na maana ya kuondoka, nakueleza kuwa ifikie wakati mashabiki wasiwe wanakariri mambo pale mtu anapoandika ujumbe wa aina kama ile, kwani si kweli kuwa anaondoka.

"Si kweli, alichokiandika hakina maana ambayo wengi wametafsiri, bado ana mkataba na Yanga na ataendelea kuwepo", amesema Ten.

Kamusoko hivi karibuni aliandika ujumbe ukieleza kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa upendo waliomuoneshea tangu ajiunge na timu hiyo.

Mashabiki wengi waliokomenti walielewa kuwa ameshaagana na mabosi wake na ikachukuliwa kuwa anaondoka Yanga.