
Adhabu hiyo imetolewa katika kikao chake cha Machi 4, 2017 iliptia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 inayoendelea hivi sasa.
Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo imesema kuwa, katika mchezo kati ya Simba na Young Africans iliyochezwa Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Young Africans iliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
"Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi, Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano)." Imesema taarifa hiyo
Kikao hicho pia kilifuta kadi ya kwanza ya njano aliyoadhibiwa mchezaji Obrey Chirwa wa Young Africans wakati timu hiyo ilipocheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu na hivyo kufuta kadi nyekundu aliyoadhibiwa.