Alhamisi , 6th Oct , 2016

Wachezaji wawili wa klabu ya Sparta Prague ya Ligi Kuu ya Jamhuri ya Czech wameagizwa kufanya mazoezi na klabu ya wanawake, baada ya maneno yao ya unyanyasaji wa kijinsia kwa mwamuzi msaidizi wa kike.

Mlinda Mlango wa Sparta Tomas Koubek, ambaye ni mmoja kati ya wawili walioadhibiwa

Tukio hilo lilitokea wakati Sparta wakilazimishwa sare ya 3-3 na Zbrojovka Brno, Jumapili iliyopita, ambapo mwamuzi msaidizi Bi. Lucie Ratajova kutoona tukio la kuotea la mchezaji wa timu pinzani na kufunga bao la kusawazisha,

Baada ya mchezo huo, Mlinda Mlango wa Sparta Tomas Koubek , amesema kuwa wanawake wanatakiwa kukaa jikoni na wasichezeshe mpira wa wanaume, maneno ambayo yalikuwa yakimlenga mwamuzi mwana mama.

Koubek na mchezaji mwenzake, Lukas Vacha ambaye aliandika kwenye mtandao kuwa mwamuzi huyo ni mpishi, wote wameomba radhi kwa maneno yao ya unyanyasaji wa kijinsia kwa Wanawake

Mwamuzi Lucie Ratajova