Jumanne , 31st Jan , 2017

Rais wa Band ya Akudo Zagreb Butamu a.k.a Sura ya Mvuto amesema sababu zinazopelekea  Band nyingi kupotea na kufa ni kutokana na wasanii hao kuwapiga 'vizinga' mapapaa na mashugamami wanaohudhuria matamasha ya band hizo.

Akudo

Akiongea kupitia eNewz ya EATV amesema anajipanga kurudisha band ya Akudo na kuwaondoa wasanii wote wanaopenda kuwazoea wateja na kuwapiga vizinga hali inayopelekea mashabiki wengi kukimbia wakiogopa kuombwa hela na wasanii.

Yaani mtu akiingia ukumbini yeye ni pombe tu, yeye ni kuombaomba watu hela, hiyo nimeisimamia siitaki tena, wanazoea watu hovyo, watu wamekuja na bajeti zao halafu wewe unawapunguzia. Nitawashauri weny mabendi mengine pia sababu watu wengi wanakimbia bendi zetu kwa sababu ya hilo”, Amesema Zagreb

Zagreb Butamu - Rais wa Akudo

Pia Rais wa Akudo amesema atahakikisha anawashauri viongozi wa band nyingine ili kuweza kuwafanyia kazi wasanii wote wanaopenda kupiga vizinga ili kuweza kuurudisha muziki wa band katika hadhi yake.