Jumatatu , 24th Dec , 2018

Mchezaji mpya wa klabu ya Yanga, Haruna Moshi 'Boban' anatarajia kuanza katika kikosi cha kwanza cha Yanga leo baada ya kibali chake cha kazi kukamilika.

Haruna Moshi Boban

Boban ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili lililofungwa mwezi huu, amejumuishwa katika kikosi cha kwanza kitakachoanza katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Tukuyu Stars.

Pamoja na Boban, pia mlinda mlango namba mbili wa klabu hiyo, Klaus Kindoki ameanza katika kikosi kufuatia Ramadhani Kabwili kuumia kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya Tukuyu Stars ni: 

1. Klaus Kindoki
2. Paul Godfrey
3. Gadiel Michael
4.Abdalla Haji
5. Kelvin Yondani
6. Fesal Salum
7. Pius Buswita
8. Haruna Moshi 
9. Heritier Makambo
10. Amisi Tambwe
11. Ibrahim Ajibu