Jumatatu , 24th Dec , 2018

Baada ya msanii wa maigizo anayejulikana kwa jina la Mikalla kusambaa picha zake kuzua gumzo mitandaoni kutokana na umbo lake, wengine wakudai kuwa amefariki na sio yeye na wengine wakiamini kuwa ndio mwenyewe.

Pichani, kulia ni Mikalla kipindi anaigiza filamu, na kushoto ni picha anazopost sasa kwenye mitandao.

Wakizungumza na www.eatv.tv, kwa nyakati tofauti mmoja kati ya waigizaji wenzake, Elizabeth Chijuba 'Nikita' amesema kuwa anaamini mwanadada huyo ndiye mwenyewe halisi, japokuwa mwili wake umepungua tofauti na awali kwakuwa amewahi kumuona mahali.

"Naamini yupo hai na atakuwa ndiye mwenyewe, nimewahi kumuona mara moja na mwili wake ukiwa kama vile, toka mwanzo alikuwa anamwili mdogo mdogo lakini sasa hivi umekuwa mdogo zaidi", amesema Nikita.

Kwa upande wake Mzee Chillo amesema kuwa ni kwa kipindi kirefu amepotea kwenye vyombo vya habari na miaka mitatu iliyopita ndipo walionana.

Mwanadada huyo amecheza filamu kadhaa, pamoja na maigizo ambapo alijizolea umaarufu kupitia tamthilia ya 'Jumba la Dhahabu' pamoja na filamu iliyomshirikisha marehemu Kanumba ya 'The lost twins', na sasa amekuwa gumzo kwenye mitandao baada ya kuonekana akiwa na umbile dogo zaidi ya awali suala linaloacha maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.