Jumatano , 11th Sep , 2019

Msanifu lugha Mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Consolata Mushi, amesema BAKITA wanaweza kupanua matumizi ya neno baharia, tofauti na maana halisi ya sasa.

Consolata Mushi amesema moja ya sababu ambayo itawafanya kuongeza maana ya neno hilo ni endapo litasambaa kwa watu wengi zaidi na litadumu kwa muda mrefu.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Breakfast cha East Africa Radio, amesema kuwa "kwa namna wanavyotumia sasa lazima tufanye tathmini, kwa sababu kama umepanua maana ni kama kiongozi umefanya jambo kwenye jamii, lazima tutathamini kwa upana wake".

"Upanuzi wa maana utawekwa kwenye kamusi kama utaleta mashiko, kama hautaleta mashiko utaachwa tu upite, kama misemo mingine inavyopita." amesema Consolata Mushi.

Kwa sasa usemi wa neno baharia umekuwa ukitumiwa na watu wengi, kwa kile wanachokieleza kuwa neno hilo, ni ishara ya mtu mpambanaji kwenye eneo fulani kwa ajili ya watu.