
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.
Akitembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na serikali, Waziri Aweso amesema kuwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za usambazaji maji kwa wananchi kwa kiwango bora ni wazi kuwa ipo haja ya kufanyika mabadiliko ya kiuongozi katika maeneo yote yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.
Akiwa ziarani katika maeneo ya Pugu na Segerea, Waziri Aweso, alipata fursa ya kutembelea mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya shilingi bilion 6.9, ikiwemo kuzindua mradi wa maji katika eneo la Segerea.