
Diego Costa
Mchezaji huyo kwa sasa yupo huru baada ya kuvunja mkataba na Atletico Madrid mwezi Disemba mwaka jana.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, amekubali kusaini mkataba baada ya kufikia makubaliano na timu hiyo ya Ureno na amesaini mkataba wa miaka miwili, na atajiunga na kikosi hicho mwezi Juni mwaka huu kuelekea msimu mpya wa 2021-22. Makubaliano ya mkataba huo yanamruhusu Costa kufanya mazungumzo na vilabu vingine kabla ya kufika mwezi Juni.
Inaripotiwa kuwa Costa amezikataa ofa za vilabu kadhaa ikiwemo Olympique Marseille ya Ufaransa, na ofa kutoka baadhi ya vilabu kutoka nyumbani kwao nchini Brazil na anaamini bado anauwezo wa kucheza soka la ushindani barani Ulaya.
Costa pia amewahi kucheza soka nchini Ureno, alicheza katika klabu ya Braga kabla ya kujiunga na Atletico Madrid mwaka 2007. Msimu huu Benifica ipo nafasi ya 3 ikiwa na alama 51 na imesalia michezo 10 kabla ya msimu kumalizika.