
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba
Mhandisi Kemikimba ametoa maagizo hayo alipotembelea mradi wa maji wa Buyango septemba 07 mwaka huu na kujionea hali ya utekelezaji wa Mradi huo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji ili malengo ya Serikali ya kuwafikishia wananchi maji yanafikiwa.
Mhandisi Kemikimba amesema kuwa miradi hiyo ilitakiwa kuwa imekamilika Mwezi Juni kwa mujibu wa mikataba hivyo kutokamilika kwa wakati inapelekea Wananchi kuendelea kupata adha ya maji tofauti na malengo ya Serikali.
“Nimejionea mwenyewe hali ya utekelezaji wa mradi huu ambao ulitakiwa kukamilika mwezi juni, ila kutokana na changamoto ambazo tayari tumeshazitatua naagiza miradi yote Mkoani Kagera ukiwemo huu ikamilishwe kabla ya Tarehe 30 mwezi huu.”- amesema Mhandisi Kemikimba