
Msitu
Akitoa ripoti ya miaka miwili ya hali ya mazingira kwa nchi mbalimbali duniani, Meneja wa Hifadhi kutoka shirika la hifadhi ya mazingira na wanyamapori duniani (WWF) Dkt Lawrance Mbwambo, amesema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kuepuka majanga ambayo yanaweza kutokea.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo Dkt Amani Ngusaru, amesema ripoti hiyo pia imebainisha kuwepo kwa kupotea kwa wanyama kwenye hifadhi za wanyamapori kutokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na kukosekana kwa malisho ya wanyama hao.
Aidha kuhusu viumbe hai, ikiwemo samaki wa baharini Dkt Ngusaro amesema nako hali si nzuri kutokana na baadhi ya samaki kutoweka na wengine kupotea kabisa.