
Akitoa taarifa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Owen Jasson amesema tayari kesi 13 zinaendelea Katika mahakama mbalimbali za Mkoa wa Rukwa, ambapo kati ya hizo kesi mbili zilitolewa maamuzi na Jamhuri kusinda kesi zote
Aidha Katika hatua nyingine Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa amesema katika chaguzi mbalimbali za ndani ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuthibiti mianya ya Rushwa na kutoa wito kuhakikisha vitendo vya Rushwa vinakomeshwa Katika chaguzi.