
Waziri mkuu Majaliwa amesema serikali iliagiza makusanyo yote yakusanywe kwa mfumo na kielektroniki na kisha kupelejwa benki lakini cha kushangaza afisa manunuzi huyo ambae awali alikua mtumishi wa Halmashauri ya wilaya Kisarawe alishindwa kufanya hivyo
Waziri mkuu Majaliwa amesema alishangazwa kuona mtumishi huyo ambaye alishindwa kupeleka kiasi hicho cha fedha benki alipewa uhamisho wa kwenda kufanya kazi katika halmashauri ya Mtwara Vijijini kitendo ambacho hakiendani na taratibu za kiutumishi.