Jumanne , 3rd Jan , 2023

Rais Dkt. Samia amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania, Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu akichukua nafasi ya Dkt. Moses Kusiluka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Rais Samia Suluhu Hassan

AidhaRais Samia amemteua Said Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa,  ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za ndani za idara hiyo

Katika hatua nyingine Rais Samia amemteua Dkt. Moses Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, akichukua nafasi ya Balozi Hussein Katanga, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa kudumu wa UN jijini New York

Na mwisho Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hussein Kattanga kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, akichukua nafasi ya Profesa Kennedy Gastorn, ambaye amerudishwa nyumbani, kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.