Jumatatu , 8th Mei , 2023

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaomboleza takribani vifo vya watu 400 waliokufa katika mafuriko kwenye wilaya ya Kalehe jimboni Kivu Kusini taarifa zinasema kuwa hadi sasa watu 300 wamezikwa.

Mkuu wa wilaya hiyo, Thomas Bakenge amesema kuwa idadi ya waliokufa imefika 401, na ilitarajiwa kuongezeka kwa sababu shughuli ya kuwatafuta wahanga imekuwa ikiendelea na Kulingana na taarifa kutoka eneo hilo, miili ipatayo 300 ya wahanga hao tayari imezikwa

Mvua kubwa ilianza kunyesha wilayani Kalehe jioni ya Alhamisi iliyopita, ikaifanya mito kuvunja kingo zake na kuzisomba nyumba nyingi katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi, na kusababisha hasara kubwa ya maisha na mali.

Afisa wa asasi ya kiraia katika eneo hilo, Delphin Birimbi amesema uharibifu wa miundombnu uliotokana na mafuriko hayo unakwamisha operesheni za uokozi.