Wamachinga wapewe kipaumbele - Waziri Bashungwa
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa, ameitaka sekta binafsi na washirika wa maendeleo kushirikiana na Serikali kuwatengenezea mazingira wezeshi wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) ili waweze kukuza biashara zao na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.