Tangazo la Burj Khalifa halijalipiwa - Msigwa
Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa, amesema kwamba serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote duniani la Burj Khalifa lililopo Dubai, bali limewekwa kuitangaza nchi kutokana na uhusiano mzuri uliopo na Umoja wa Falme za Kiarabu.

