Achomwa moto na rafiki yake kisa mke
Daud Emanuel (27) mkazi wa Chamwino Manispaa ya Morogoro, amenusurika kifo baada ya kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kuchomwa moto na rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Marko Gerald, baada ya kumtuhumu kuwa anajihusisha kimapenzi na mke wake.