CCM yaanza mchakato kumpata Spika wa Bunge
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mchakato wa kumpata spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao utaanza Januari 10, 2022 kwa wenye nia kuchukua fomu, na kuhitimishwa mwisho wa mwezi kwa wabunge wa chama hicho kupiga kura za kumpitisha mgombea.