Auawa na mganga akitaka kufukia milioni 9
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wawili akiwemo dereva wa pikipiki na mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumuua na kisha kumfukia mwanamke aliyekuwa ameenda kuzindika fedha za biashara kiasi cha shilingi milioni 9.

