Nimetimiza ndoto kufunga bao kwenye UCL- Elanga
Mshambuliaji kinda wa Manchester United Anthony Elanga amesema ametimiza ndoto kufunga bao kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kufunga bao dhidi ya Atletico Madrid, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora mchezo ambao umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

