Operesheni yabaini 'madudu' Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amesema operesheni iliyofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama katika kata ya Mabwepande, Januari 24 na 25, mwaka huu imewakamata watuhumiwa 314 wa uhamihaji haramu na baada ya mahojiano watu 84 pekee ndiyo waliobainika ni wahamiaji haramu.