
Aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.
Hapo awali, Mtolea aliwahi kusema kuwa kitendo cha Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia kuhamia CCM ni afadhali kwa kuwa ameamua kuweka wazi mapenzi yake dhidi ya CCM kuliko kujificha ndani ya Upinzani huku akifanya kazi za chama hicho.
Mtulia alisema "Sababu za kujiuzulu ni kutokana na uzoefu nilioupata kwa miaka miwili ya ubunge wangu ambapo nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza.
Kupitia mahojiano maalumu aliyowahi kufanya na www.eatv.tv, Mtolea alisema hadi kufikia hatua ya mtu kuondoka chama kimoja kwenda kingine huwa ni maamuzi ya muda mrefu ambayo mtu huwa anayafanya ikiwa ni pamoja na kuwa na mapenzi na chama anachohamia.
"Hakuna mtu ambaye anafanya maamuzi ya kusema leo mimi ninakwenda CCM ikawa leo leo ndiyo amefikiria na leo leo ndiyo amekipenda na leo ndiyo anafanya maamuzi, ni lazima itakuwa amekipenda muda mrefu, au mtu akiamua akaoe au kuolewa ina maana amekaa uchumba na mtu huyo kwa muda mrefu.
Mtolea alitangaza kujivua nafasi yake ya ubunge kupitia Chama Cha Wananchi CUF, Nov 15 mwaka huu kwa kile alichokieleza juu ya uwepo kwa mgogoro wa kiuongozi baina ya pande mbili za viongozi wa Chama hicho ikiwemo upande unaoungwa mkono na Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Seif.
Aidha wakati akitoa maelezo yake kwa Wabunge siku ya kujiuzulu nafasi yake na kujiunga na CCM, Mtolea alivikaribisha vyama vingine vya siasa nchini kufanya naye kazi akidai bado anatamani kuendelea kuwatumikia wananchi wa Temeke na baadaye alitambulishwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally.
Hata hivyo Jana kupitia Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kilimtangaza Abdallah Mtolea kuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Temeke kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema Januari 2019.