
Mkurugenzi wa kitengo cha Utafiti na ubora wa Mifumo kutoka Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bwana Benny Mallya katikati,upande wa kulia ni Silvester Omary Afisa habari kwa Mkemia Mkuu na Frank Mvungi kushoto Afisa Habari Maelezo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini Tanzania imesema katika kipindi cha mwaka mojaa jumla ya matukio na ajali za Kemikali 11 ambazo zilitolewa taarifa na kusababisha vifo vya watu 14 pamoja na uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua kwa moto magari na tani zaidi ya 250 za Kemikali.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Ubora wa Mifumo kutoka Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bw. Benny Mallya ametoa takwimu hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu sheria ya usimamizi na uthibiti wa kemikali sura 182, na kuainisha kuwa kufuatia na taarifa hizo na kubaini chanzo cha ajali hizo ni kukosekana kwa uelewa juu ya hatari na madhara yanayoweza kusababishwa na kemikali hizo.
Amesema ili kukabiliana na madhara yanayotokana na matumizi yasiyo salama ajali na matukio ya kemikali Serikali iliamua kutunga Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani sura 182 lengo kuu la sheria hiyo likiwa ni kuhakikisha kemikali zinatumika katika hali salama bila kuleta athari kwa watu na mazingira.
Kuhusu gharama kubwa zinazolalamikiwa na wahitaji wa vipimo vya DNA Bw. Mallya amesema kuwa tataizo la kifedha ndio linakwamisha suala hilo lisifanyike kwa muda uliopangwa.