Monday , 8th Jan , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira amewamwagia sifa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambao walikwenda kula sikukuu za mwisho wa mwaka mkoani humo, kwa kufanya matumizi makubwa na kuongeza pato kwenye uchumi wa mkoa huo.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv mama Mghwira amesema wakazi hao walifanya matumizi makubwa kufurahia sikukuu hizo, licha ya watu wengi kuamini kuwa hali ya uchumi imebana (vyuma vimekaza).

Mama Mghwira amesema alipata fursa ya kutembelea maeneo ya starehe kwa siku za sikukuu hizo, na kuona jinsi gani biashara zilikuwa zikienda vizuri, ikiwemo maduka ya nguo na bar mbali mbali.

Msikilize hapa chini