Thursday , 6th Oct , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhirifu na kutumia madakaraka yao vibaya.

Mrisho Gambo

Gambo ametoa maagizi hayo wakati akiongea na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo ambapo amesema amechukua hatua hiyo ili iwe fundisho kwa wataalam na watumishi wengine katika mkoa wa Arusha.

Mkuu huyo wa mkoa amesema watumishi wengi wamekuwa wanafanya kazi kimazoea bila kuwajali wananchi wanaowahudumia ambapo amesema watumishi hao wamekuwa wazembe na kuisababishia hasara halmashauri hiyo.

Aidha Mrisho Gambo amemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo arejeshwe katika halmashauri hiyo ili kujibu tuhuma zinazomkabali ikiwemo kufanya manunuzi kinyume cha sheria pamoja na kuingia mikataba kwa maslahi binafsi.