Monday , 10th Oct , 2016

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa wizara yake itasimamia mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika mji wa Nansio baada ya kubaini kuwa halmashauri ya Ukerewe haina uwezo wa kuendesha mradi huo.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake mkoani Mwanza katika wilaya ya Ukerewe ambapo amesema mradi huo wa Nansio umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 13 kwa hiyo uamuzi wa unalenga mradi huo unatoa huduma endelevu kwa wananchi.

Akibainisha hayo mbele ya vingozi na wataalam wanaosimamia sekta ya maji wilayani Ukerewe amesema kuwa amebaini uwezo mdogo wa Halmashauri katika uendelezaji wa maradi huo hali ambayo inaweza ikafanya miundombinu ya mradi huo kuharibika haraka.

Aidha waziri huyo wa maji amesema suala lingine ni kubainika kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya serikali zinazotolewa kutumika kinyume na matakwa ya serikali na kushindwa kuendeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Ukerewe.