Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea.
Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, Wakili wa serikali Beatrice Nsana amedai kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Julai 3 mwaka huu.
Hata hivyo, Mhe. Kubenea ambaye anatetewa na Mawakili watano amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhaman hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena Julai 26 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokamilika.




