Saturday , 11th Mar , 2017

Hospitali Kuu ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya imetangaza kuwafukuza kazi madaktari 12 na kuwapa wengine 48 adhabu kali kwa kuendelea na mgomo.

Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini Kenya

Hata hivyo madaktari hao wamesema hawatakata tamaa katika harakati zao za kudai haki yao na kuuonesha umma wa Kenya ukweli kuhusu mgogoro wao na serikali.

Mapema wiki hii Mahakama iliwaamuru Magavana na serikali kuafikiana na kutia saini takabadhi tatu ambazo ni muhimu katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo.

Lakini baadaye katika kongamano la kujadili ufanisi na changamoto za mfumo wa ugatuzi wa madaraka mjini Naivasha, Rais Uhuru Kenyatta na Gavana Peter Munya kwa niaba ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti waliwashutumu vikali madaktari kwa kuendelea na mgomo uliozorotesha sekta ya afya nchini humo.