Monday , 21st Nov , 2016

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam imewakamata watuhumiwa zaidi ya 10 wakiwa na Bastola nne ,Browning 1 namba A731441, Revolver 2,Glock 19 yenye namba ELS377, milipuko 6 na risasi 16.

Kamishna wa Polisi Simon Sirro

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam CP Simon Sirro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutoka sehemu mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam katika msako uliofanywa na kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha.

Silaha hizo zimekamatwa maeneo ya Mbande,Yombo ,Tambuka ,Chang'ombe na watuhumiwa wako chini ya ulinzi wa Polisi kwa mahijiano zaidi..

Katika tukio lingine Kamanda Sirro amesema polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 5 na pombe bandia aina ya Konyagi na vifaa vya kutengenezea kinywaji hicho.

Kuhusu ripoti ya madawa ya kulevya amesema bado utaratibu unafanyika wa kukabidhiana majina ya wahusika na pindi taratibu hizo zitakapokamilika jeshi hilo litatoa taarifa yake.

Kuhusu watuhumiwa wanaoujihususha na biashara ya Sisha Kamanda Sirro amesema tayari wamewakamata watuhumiwa 3 katika wilaya ya Kinondoni na hatua za kiusalama zinaendelea kufwata ili kuwafikisha mahakamani.

Kwa upande wa tozo ya makosa ya usalam barabarani Kamanda Sirro amesema wamefanikiwa kukusanya Shilingi 414,060,000 katika kipindi cha siku nne kuanzia tarehe 17 hadi 21 Novemba