Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Matokeo ya kidato cha pili, darasa la nne kufutwa

Monday , 12th Nov , 2018

Baraza la mtihani la taifa (NECTA), limesema kuwa halitosita kuvifuta vituo ambavyo vitahatarisha usalama wa mitihani ya taifa inayoendelea nchini kwa kidato cha pili na darasa la nne, pamoja na kufuta matokeo ya watahiniwa.

Katibu mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde.

Hayo yamebainishwa na Katibu mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde ambapo amesema kuwa, watakaohusika na kukiukwa kwa kanuni za mitihani watawajibishwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

"Watahiniwa watambue kuwa kukiuka kanuni za upimaji au kufanya udanganyifu kutafanya wafutiwe matokeo yao yote, lakini pia Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa upimaji wa taifa", amesema Dkt. Msonde.

Wanafunzi wa kidato cha pili wameanza mitihani yao leo Novemba 12, kote nchini na watamaliza Novemba 23, huku wanafunzi wa darasa la nne wao wataanza tarehe 22 na 23 mwezi huu.

Hayo yanajiri ikiwa ni miezi michache tu tangu Baraza hilo lilipofuta matokeo ya darasa la saba kwa baadhi ya shule nchini kutokana na udanganyifu, ambapo shule zilizofutiwa ni, shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao