Friday , 24th May , 2024

Mama mdogo wa Penina Method, mwanamke aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na mpenzi wake kisa wivu wa mapenzi ameiomba serikali imchukulie hatua kali kijana aliyetambulika kwa jina moja la Joseph ambaye ndiye mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Joseph na Penina

Akizungumza na #EastAfricaTV ndugu wa marehemu Penina, amedai kuwa marehemu na mpenzi wake walikuwa na mpango wa kufunga ndoa mwezi Julai mwaka huu.

Mtuhumiwa wa tukio hilo alijisalimisha jana polisi baada ya kufanya mauaji majira ya saa 12 alfajiri kwenye baa ya mpenzi wake huyo ambaye anadaiwa hakurudi nyumbani usiku wa kuamkia siku ya tukio.

Penina ameacha watoto wawili na mwili wake unazikwa leo jioni Goba Dar es Salaam.