Wednesday , 16th Jan , 2019

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonesha kuunga mkono muswada mpya wa vyama vya siasa ambao umekuwa ukilalamikiwa na na vyama vya upinzani nchini kwa kile kinachodaiwa kuwa kinampa mamlaka makubwa Msajili wa vyama kuratibu masuala ya ndani ya chama cha siasa.

Akizungumza kwenye mkutano uliowahusisha wanachama wa CCM na wananchi ili kujadili muswada huo kabla haujafikishwa bungeni, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amedai muswada huo umetokana na mapendekezo ya wananchi.

"Sisi kama chama tunaunga mkono kuelezwa kwa majukumu ya Msajili wa vyama vya siasa, kwenye muswada mpya", amesema Polepole.

"Muswada huo umetokana na mapendekezo ya wananchi, kwa sababu sheria ya sasa itatufanya kukua, kutusaidia masuala yote ya haki hayatakuwa na mzaha, kuhakikisha viongozi wa kisiasa hawatumii vyama vyao vibaya", amesema Polepole.

Mwishoni mwa mwaka jana wakiwa visiwani Zanzibar, Vyama vya upinzani nchini walitoka na maazimio ya kupinga muswada mpya wa sheria ya vyama vya siasa.