
Waziri Mwigulu ambaye wizara yake ndio ina dhamana ya kusimamia amani na usalama wa raia na mali zao nchini ametoa salamu zake za sikukuu huku akiwakumbusha wananchi kuzingatia Amani.
Kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mh Mwigulu ameandika, “Merry Christmass & Happy New Year, tusherekee kwa Amani na Upendo”.
Mbali na Waziri Mwigulu kusisitiza Amani kipindi hiki cha sikukuu, hivi karibuni pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu bila kuvunja sheria za nchi.