Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kuweka mazingira yatakayowawezesha wanafunzi wenye uwezo wa kusomea masomo ya Sayansi katika elimu ya Sekondari kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ili kuwa na wanasayansi wengi zaidi nchini wataoimarisha ukuaji wa viwanda.
Hayo yamebainishwa leo na serikali wakati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kikifungua Maonesho ya Tafiti za vitivo mbalimbali vya chuo hicho yatakayodumu kwa siku tatu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Prof. Adolf Mkenda anasema kumekuwa na wanafunzi waliobobea katika ubunifu wa teknolojia inayowezesha viwanda kuimarika.
Ukuaji wa uchumi wa nchi unategemea uwekezaji mkubwa uliofanywa katika teknoloji, Prof. Adolf Mkenda amewataka wanafunzi kupenda zaidi masomo ya sayansi ili kuwa na wataalam wa kutosha.
Dkt. Egid Mubofu ni Mkuu wa Idara ya Kemia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema wamefanya utafiti na kubuni vifaa vinavyotumika kwenye vifaa vya elektroniki ikiwa ni pamoja na simu za mkononi.