Sunday , 1st May , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa serikali yake imejipanga kuwashughulikia watumishi wa umma ambao ni wezi, mafisadi, wala rushwa na wazembe na kuahidi kuwa atawashugulikia mahali popote walipo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa serikali yake imejipanga kuwashughulikia watumishi wa umma ambao ni wezi, mafisadi, walarushwa na wazembe na kuahidi kuwa atawashugulikia mahali popote walipo.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika Mkoani Dodoma ambapo ameeleza kuwa hadi kufikia jana serikali imebaini kuwapo watumishi hewa 10,295, ambao walikuwa wakiigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 11 kila mwezi.

Dkt. Magufuli amesema fedha hizo za malipo ya watumishi hewa ni nyingi mno ambapo zigeweza kusaidia shughuli mbalimbali za maendelo na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali za afya, elimu na hata kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Akizungumzia suala la kupunguza mishahara mikubwa ya watumishi wa umma Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake mshahara mkubwa utakuwa ni shilingi milioni 15 tu, na kwa wale waliozoea mishahara ya shilingi milioni 30 kama hawataki kazi waache hata leo.

Aidha, Dkt. Magufuli amesema ili kumpunguzia mzigo wa kodi mfanyakazi serikali yake imepunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi (PAYE), kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 kuanzia mwaka wa fedha wa 2016-2017.