
Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, kwa niaba ya wabunge wenzake Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema hatua ya kuvunjwa kwa kamati hizo kuna lenga kutokaa pamoja na Mkaguzi wa hesabu za serikali bungeni
John Mnyika amesema uamuzi wa kutangaza kuwa hawawezi kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad hawaukubali kuwa hauna tija kwa Taifa.
“Kwanza ni kwa nini asisubiri kwanza CAG aitwe na Kamati ya Maadili ahojiwe juu ya kauli yake ndipo ajue cha kumfanya, lakini yeye ameamua kwenda mbali zaidi na kuzuia kufanya kazi na taasisi nzima ambayo ni jicho la Bunge na Watanzania,” amesema Mnyika.
Bofya link hapo chini kusikiliza zaidi.