Friday , 13th May , 2016

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imesema shilingi bilioni 4,128,000,250 zimetumika kununua vifaa tiba katika hospitali mbalimbali za rufaa nchini ili kufanya maboresho ya hospitali hizo

Kigwangala akifafanua jambo Bungeni mjini Dodoma

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imesema shilingi 4,128,000,250 zimetumika kununua vifaa tiba katika hospitali mbalimbali za rufaa nchini ili kufanya maboresho ya hospitali hizo katika kuondokana na huduma za afya kufanyika nje ya nchi ambazo zimeigharimu serikali shilingi 32, 856,000,000 tangu mwaka 2012.

Hayo yameelezwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge Mhe. Ruth Hiyobu Molel aliyetaka kujua gharama zilizotumika kwa wagonjwa kutibiwa nje pamoja na juhudi za serikali za kuboresha hospitali za rufaa nchini.

Akizungumzia kuboresha huduma za afya katika Zahanati, Dkt. Kigwangala amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa watumishi 150 wanaowahudumia mama wajawazito wenye kisukari katika vituo vya afya, pamoja na kutoa vifaa tiba ili wagonjwa wa kisukari wahudumiwe katika vituo vidogo tofauti na ilivyo sasa wanahudumiwa katika hospitali ya ngazi za Wilaya na Mkoa.