Friday , 24th Apr , 2015

Serikali imetakiwa kushirikisha wananchi katika masuala ya mazingira ili kufanya mazingira yawe endelevu kwa kutumia taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini na taasisi nyingine zinazohusu mazingira.

Moja ya mizinga ya nyuki inayotengenezwa hapa nchini

Afisa mistu manispaa ya iringa Hobokelo Mwambeso akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kulinia asali katika vikundi sita vilivyopo kata ya kihesa vinavyofuga nyuki katika mlima wa mafifi amesema kuwa wananchi pia wanapaswa kujishugulisha na si kutegemea serikali iwatendee.

Afisa huyo pia amewataka wananchi kuunda vikundi mbalimbali ambavyo vitaweza kuwaletea maendeleo katika maeneo yao kwa kufuata utaratibu wa mansipaa ambao ni kusajiriwa kwa vikundi hivyo kabla ya kuanza kazi ili waweze kupewa kibali pamoja na maeneo ya kufanyia shughuli zao.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi katibu wa kikundi cha kimama Clayson Kinyala amewataka wanavikundi hao kuyapa masuala ya mazingira kipaombele zaidi ili mkurugezi aweze kuwa na moyo wa kuwatafutia wahisani watakao wasaidia.

Hata hivyo amewataka wanavikundi kuziunga mkono taasisi zinazowasaidia katika masuala ya utunzaji wa mazingira na ufugaji wa nyuki.