Thursday , 28th Apr , 2016

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka huu George Mbijima, amewataka Watanzania hasa vijana kuwa waadilifu na wachapakazi katika ajira zao ili kuwavutia waajiri wao wakiwemo wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kukuza uchumi wa taifa

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka huu George Mbijima,

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge ametoa kauli hiyo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga,wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakombo ambapo pamoja na mambo mengine amesema hatua hiyo itawasaidia kufanya kazi vizuri na kuwaondoa katika lindi la Umasikini.

Mbijima amesema kuwa vijana wanapopata ajira ni lazima wabadilike kimatazamo na kuacha udokozi na ubadhilifu wa fedha katika miradi jambo ambalo huwa linawakatisha tamaa waajiri kiasi ambacho kinafanya wawekezaji wengi kuajiri wageni kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa wageni wengi kutoka nchi za Jumuiya za nchi afrika Mashariki hasa Kenya na Uganda wanafaidika na Soko la pamoja la Ajira nchini Tanzania kutoka na wengi wao kuaminika na waajiri nchini kwetu kushinda wazawa hata kwa kazi ambazo zinaweza kufanya na Watanzania ikiwemo mahotelini.

Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Mjini Bi. Mary Chatanda, amewaomba vijana kurejesha mikopo wanayokopa kwenye vikundi ili iwanufaishe wengi zaidi kwa kuopeshwa vijana wengine ambao wanauhitaji wa mikopo hiyo.

Nae Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bi. Hafsa Mtasiwa, amewaomba madiwani kusimamia kikamilfu fedha za mikopo zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya vijana ili kutimiza lengo la kutenga asilimia kumi kwa vijana na Wanawake.

Sauti ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka huu George Mbijima,