Mwakilishi wa vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) nchini Kenya Hanna Wanja Maina.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa vijana wa Shirika la Umoja wa Kataifa la Kuwahudumia Watoto UNICEF nchini Kenya Hanna Wanja Maina akiwa mjini Istanbul Uturiki ambapo amesema wanawake na walemavu huwa wanapata shida ya kujiokoa pindi vurugu zinapotokea katika nchi.
Hanna amesema kuwa katika kongamani hilo ambalo pia limeshirikisha watu maarufu wakiwemo wanamuziki amesema nao wananafasi kubwa katika kulinda amani katika jamii ili kunusuru majanga hayo ambayo huwa yanatokea na kuathiri wanawake, na walemavu.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali ya Kenya inapaswa kufukiria kwa kina ikiwa ni pamoja na kuwa na mipango madhubiti ya kuwasaidia wakimbizi ambao wengi wao ni wanawake pale wanapotarajia kufunga kambi za wakimbizi nchini humo ikiwemo kambi kubwa ya Daadab.