Thursday , 6th Oct , 2016

Watanzania wametakiwa kubadilika na kuanza kutumia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ili kuachana na usumbufu wa kulazimika kusafiri umbali mrefu sambamba na kutumia gharama kubwa kufuata huduma za kifedha katika matawi ya benki husika.

Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Christina Manyenye (kushoto) akizungumza na wanahabari hawapo pichan

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Christina Manyenye wakati akizungumzia huduma mpya iliyopewa jina la JIULIZE KWA NINI, huduma inayolenga kupunguza usumbufu kwa wateja wa benki hiyo popote pale walipo.

Kwa mujibu wa Bi. Christina, benki na taasisi za kifedha hivi sasa zinahama kutoka katika utaratibu wa zamani wa kutoa huduma zao katika ofisi na matawi na kuelekea kwenye utoaji wa huduma hizo kwa njia ya mtandao na kwamba Watanzania hawana budi kubadilika kuendana na mabadiliko hayo.