Friday , 24th Apr , 2015

Viongozi wa kidini wametakiwa kuwapa waumini matumaini ya kuwa wanaweza kuwalea watoto wao na kuwapatia misingi imara ya kiroho na kimwili tangu wanapokuwa wadogo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenburg Mdegela.

Askofu wa kanisa la kiinjili la KKKT Dayosisi ya Iringa Dk. Owdenburg Mdegella akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua kituo cha malezi cha watoto wadogo kilichomo katika kituo cha Huruma Center mtaa wa kigamboni manispaa ya Iringa.

Askofu amewataka wachungaji katika sharika zote za Dayosisi ya iringa kutoanzisha miradi ambayo haimjengi mtu kiroho na badala yake waanzishe miradi inayowawekea misingi ya kiroho kuanzia utotoni hususani vituo vya malezi ya watoto wadogo.

Aidha ameeleza kuwa watoto hawatendewi haki pale wanapoachwa na wadada wa kazi kutokana na kuwa kuna vitu vya msingi ambavyo hawavipati kutoka kwa walezi hao hivyo amewataka wazazi kuwaleta watoto wao kwenye kituo hicho cha malezi cha Huruma Center.

Hata hivyo akisoma risala mlezi wa kituo hicho Bi. Constansia Chilewa amesema kuwa kituo kwa ujumla kimegharimu shilingi milioni ishirini laki tatu na sabini na nane elfu na fedha hizo zote ni kutoka kwa wafadhili kutoka St.Paul kutoka nchini marekani.