Saturday , 16th May , 2015

King of the Best Melodies, Christian Bella, msanii wa muziki wa dansi anayeifanya vizuri pia game ya Bongo Fleva, amesema kuwa kuna umuhimu wa wasanii hususan wa kike kujiheshimu zaidi kupitia sanaa zao, na kuuza zaidi kazi na sio muonekano.

Christian Bella

Kauli ya Bella inakuja kufuatia mjadala mkubwa wiki hii kuhusu suala la wasanii kulinda heshima na maadili kupitia kile wanachokifanya, ambapo mkali huyo amesema kuwa ni muhimu kuweka sanaa mbele, kwa vile kipaji cha mtu hakijifichi hata kama ana ulemavu.

Bella amekazia kuwa, suala la maadili kwa wasanii wa kiume si tatizo kabisa, akiwataka wasanii wa kike kufahamu kuwa ni muhimu kujiheshimu, wengine wakiwa ni dada na mashemeji, mahusiano ambayo huhitaji kuwekeana staha na kutoruhusu baadhi ya vitu ama viungo kuonekana hadharani.