Thursday , 20th Dec , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Pol, ametekwa kimapenzi na msichana tajiri wa Kikenya, anayejulikana kwa jina la Anerlisa Muigai.

Msichana huyo ambaye ni CEO wa kampuni ya Nero inayotengeneza maji ya kunywa, amemfanya Ben Pol kuwa njiwa kwa kuruka hewani kila siku kwenda nchini humo, ili kumuona mpenzi wake huyo.

Ingawa wenyewe hawajaweka wazi rasmi, lakini ukaribu wa wawili hao umezidi kutia shaka na wengine kupigia mstari kuwa kaka yetu sasa hafurukuti kwa msichana huyo mkali na mwenye mkwanja mrefu nchini humo.

Wawili hao wameshaonekana sehemu mbali mbali nchini Kenya wakiwa pamoja, na hivi karibuni wamesafiri pamoja kwenda nchini Vietnam kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Hata hivyo kitu usichokijua ni kwamba licha ya kuonekana ana umbo zuri la kuvutia, mwanadada huyo alikuwa mnene kiasi cha kuweza kumfikia muigizaji wa Bongo Movie Asha Boko, lakini aliamua kupungua kwa namna ambayo wengi waliamini kuwa alifanya upasuaji, huku mwenyewe akidai kwamba alizingatia tu ulaji wenye afya.

Angalia hapa chini wanavyokula bata.

Ben Pol akiwa kwenye ndege na Anerlisa
Anerlisa kabla ya kupungua uzito