Monday , 11th Jul , 2016

Mkongwe Dudubaya a.k.a Mamba amekuwa akionekana kuzungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii zaidi kwa issue mbalimbali nje ya muziki.

DUDUBAYA

Enews ilitaka kujua imekuaje DUDU anatrend mitandaoni bila ya kuwa na ngoma??

Katika mazungumzo yake na Enews, Dudu amesema "muziki si mkojo kuwa ukijisikia unakojoa inatakiwa ujipangea vizuri ili unapotoa wimbo ukae muda mrefu na uwe unaeleweka pia kitu ambacho vijana wengi wa sasa hawana".

Lakini pia Dudu akijibu tuhuma za kuwa kipindi anahit na Dar Skendo alikuwa mbinafsi kwa kufanya ngoma peke yake hadi kusababisha kundi kusambaratika, amesema si kweli ila ilikuwa ni ubunifu wake pekee.